Sunday, 19 June 2016

DR SIMON WALTON AMALIZA MUDA WAKE KUKITUMIKIA KITUO CHA AFYA CHA KANISA ANGLIKANA DAYOSISI YA DSM KILICHOPO BUGURUNI.

Familia ya Dr Simon ikiwa katika hafla ya kumuaga.


Ni kwa Neema tu,Dr Simon akicheza na baadhi ya wafanya kazi kituo cha Afya cha kanisa Anglikana Buguruni.

Dr Simon Walton aliwasihi wafanya kazi kufanya kazi kwa upendo na ushirikiano.Anatarajia kurudi nchini Uingereza hivi karibuni.

Dr Simon Walton akiwa na Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Dayosisi Ndugu Yohana Sanga.

Dr Simon akijaribu shati moja ya zawadi alizozawadiwa na wafanya kazi.

Saturday, 18 June 2016

KANISA ANGLIKANA DAYOSISI YA DAR ES SALAAM KATIKA MKAKATI WA KUANZISHA RADIO.

Mkurugenzi wa Azam Televisheni Ndugu Tiddo Mhando kushoto na Mtangazaji Mahiri Charles Hilally kulia pamoja na wajumbe wengine wakishiriki kikao cha uanzishwaji wa Radio ya Dayosisi.

Katikati ni Mwenyekiti wa kikao cha uanzishwaji Radio ya Dayosisi Ndugu Leonald Malango akiongoza kikao

Kulia Mtangazaji wa Azam Televisheni ndugu Charles Hilally akifuatilia kwa makini kikao.

Kushoto Mkurugenzi wa Azam Televisheni Ndugu Tiddo Mhando akifuatilia kikao hicho.

Katikati Mhashamu Baba Askofu Dr Valentino Mokiwa akiongoza kikao cha wajumbe wa kamati mbalimbali zililzotokana na maagizo ya Mkutano wa Sinodi ya 19.

Baadhi ya wajumbe mkakati uanzishwaji Radio.

Kushoto Afisa Habari wa Dayosisi Ndugu Yohana Sanga akiwa na baadhi ya wajumbe.