Thursday 22 October 2015

MATANGAZO

MAANDALIZI YA KALENDA.


Ofisi ya Dayosisi inaomba Mitaa kuleta picha Idara ya Habari hapa Dayosisi kwa ajili ya kuandaa Kalenda ya mwaka 2016 kabla ya tarehe 30 Nov 2015.

ALMANAC.


Ofisi ya Dayosisi imeanza kuandaa ALMANAC ya mwaka 2016.Mitaa inaombwa kuwasilisha ratiba za matukio kabla ya tarehe 30 Nov 2015,hapa Idara ya Habari na Mawasiliano Dayosisi .

BIMA


Pia Dayosisi inawatangazia waumini na Watanzania wote kuwa Idara yake ya Bima (ANGLO INSURANCE AGENCY) imeendelea kutoa huduma zake za bima za kawaida na maisha(General and life assurance)ikiwemo bima za magari,nyumba,afya,biashara,elimu,maisha,ajali,majaliwa,n.k.

                          KARIBU UPATE HUDUMA BORA.

KITUO CHA AFYA BUGURUNI ANGLIKANA CHAZIDI KUBORESHA HUDUMA ZAKE ZA AFYA.




Mtoto akipimwa uzito



Mkurugenzi wa kituo cha Afya Buguruni Anglikana DR Simon Walton.
Mmoja wa Madaktari wa kituo hicho akifanya vipimo katika maabara.

Moja ya chumba kilicho katika matayarisho ya utoaji wa huduma za upasuaji.

Sunday 11 October 2015

MAVUNO YA UMAKI

NAOMBA BEI
Mratibu wa Umoja wa wanawake (UMAKI) wa Dayosisi Bi.Edina Mdoe akiinadi saa wakati wa sikukuu ya Mavuno katika kanisa la Kristo Ni Mfalme Kinondoni



                        MAMA NI LANGO LA BARAKA
Father Napera akiendesha ibada ya sikukuu  ya mavuno,ambapo katika ujumbe wake alisisitiza kuwa mwanamke ni nguzo ya pekee katika maendeleo ya Familia

Tuesday 6 October 2015

HONGERA CANON LUGENDO.


Kanon Julius Lugendo akipongezwa na waumini wa kanisa la Mt Paulo Ukonga baada ya kuteuliwa kuwa Askofu wa Dayosisi ya Mbeya.