Sunday 24 July 2016

Marafiki wakipaka rangi jengo la kituo cha watoto yatima.

Gari lilitolewa na Dayosisi kusaidia kituo cha Yatima likiwa katika hali nzuri baada ya kukarabatiwa.

Kituo hicho pia kinaendesha miradi mbalimbali ikiwemo bustani za mboga na ufugaji.

Ma Sister ambao ndio walezi wa kituo cha yatima wakishiriki michezo na watoto hao pamoja na marafiki.





ZIARA YA MARAFIKI TOKA NCHINI MAREKANI KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA VALENTINE CHILDRENS HOME KILICHOPO BUZA DSM.WAIOMBA JAMII KUWA NA MOYO WA UPENDO KWA WATOTO HAO NA KUWASAIDIA.

Mmoja wa marafiki akiwa amembeba mtoto yatima.


Marafiki toka nchini Marekani wakiwa na watoto yatima baada ya kwenda nao eneo la michezo la FUN CITY Kigamboni ambapo walicheza nao,wakala na kunywa.



Afisa Habari wa Dayosisi Yohana Sanga kushoto akiwa na mmoja wa marafiki.

Monday 18 July 2016

WANANCHI WALISHUKURU KANISA ANGLIKANA DAYOSISI YA DAR ES SALAAM KWA HUDUMA YA MAJI.

Canon Howard Castlebery toka nchini Marekani akizindua kisima kilichopo Tuangoma ambacho amekifadhili kupitia Dayosisi ya Dar es salaam.

Katibu mkuu wa Dayosis Canon Jonathan Shenyagwa katikati  akizungumza na mkuu wa shule ya Sekondari Minaki  kulia Mwl Harold Chungu katika ziara ya uzinduzi wa kisima.


Canon Joseph Opiyo akizindua kisima kwa maombi shule ya Sekondari Minaki Kisarawe Dsm.


Canon Howard akizindua kisima.


Kisima kimezinduliwa


Bwawa la maji yaliyokuwa yanatumiwa na wanafunzi wa Minaki na wakazi wa Kisarawe ambayo si salama kwa matumizi ya binadamu.

Katibu mkuu wa Dayosisi akisalimiana na waamini wa Kianglikana kanisa la Damu ya Yesu takatifu lililopo Ruvu Stesheni kabla ya uzinduzi wa kisima.

Kisima kikifanyiwa maombi


Kigango cha Damu ya Yesu takatifu ambacho waamini wake walio wengi wana asili ya kimasai.Katibu mkuu pamoja na wafanya kazi wa Dayosisi waliokuwa katika ziara hiyo wamejitolea mifuko ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa Kigango cha kisasa.


Huduma ya uchimbaji kisima ikiendelea katika kijiji cha Kisezi wilaya Bagamoyo
Wananchi wa kijiji cha Kisezi wakilishukuru kanisa.

Sunday 17 July 2016

IBADA YA KUSIMIKA MA CHAPLAIN ARCHIDIKONARI YA ILALA KATIKA KANISA LA MT THOMAS YOMBO.





Canon Jerome Napella akiongoza Ibada ya kuwasimika Ma Chaplain katika kanisa la Mt,Thomas Yombo.


Sehemu mojawapo ambayo inahitaji utaalamu na umakini katika upigaji wa vyombo vya muziki ni DRUMS.Mtoto Jonas Malogo 14 wa kwaya ya Anglikana Mt Paulo Ukonga amekuwa mahiri katika upigaji DRUMS pindi kwaya iimbapo.