Thursday, 29 December 2016

MATUKIO MISA YA X MAS NA UTOAJI MISAADA KITUO CHA WATOTO YATIMA.

Askofu  Dr Valentino Mokiwa akimvisha kiatu mmoja wa watoto yatima wa kituo cha Valentine kilichopo Buza Dsm ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na akina Mama wa Kikristo wa kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam.[UMAKI.]

Askofu Mokiwa Akiendesha misa ya Xmas Kanisa la Mt.Cesilia Kinyerezi iliyokwenda sambamba na kupandisha Kigango hicho na kuwa mtaa kamili.

Umoja wa akina mama wa Kikristo Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam wakitoa msaada kituo cha watoto yatima kinachomilikiwa na kanisa Anglikana.


Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam latekeleza sera ya upandaji miti jiji la Dar es salaam.

Askofu Dr Valentino Mokiwa akiwa na Askofu mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania Jacob Chimeledya [kushoto]na mwakilishi toka ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam na baadhi ya watumishi wa Dayosisi wakiwa katika mazungumzo katika zoezi la upandaji miti lililofanyika viwanja vya kanisa kuu Mt.Albano Upanga Dec 2016.







Askofu Mokiwa akishirikiana na mwakilishi ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam katika zoezi la upandaji miti.

                                                               NAFASI ZA KAZI.
Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam inakaribisha maombi ya nafasi za kazi zifuatazo.
1,Mkuu wa shule ya Sekondari Buza
2,Mkurugenzi wa fedha wa Dayosisi.
3,Afisa Bima,Anglo Insuarance


Kwa maelezo zaidi fika ofisi ya Dayosisi makao makuu Ilala Amana mtaa wa Moshi au piga simu no 0713,233573.Mwisho wa kupokea maombi ni Februari 2017.