Sunday, 27 September 2015

IBADA YA KIPAIMARA

BWANA AKUBARIKINI NA KUWALINDA.

Askofu Dakta Valentino Mokiwa akiendesha ibada ya Kipaimaira katika kanisa la Mt Philipo lililopo Ukonga Mazizini jijini Dar-er-salaam ambapo katika ujumbe wake aliwasihi waumini kuishi maisha matakatifu ili kujenga familia zenye watoto wenye hofu ya Mungu.
                                                          MBUZI  WA SUPU.
Askofu Mokiwa akipokea zawadi ya mbuzi toka kwa wazee wa kanisa la Mt Philipo lililopo Ukonga Mazizini jijini Dar-er-salaam.
TUMEKUELEWA BABA ASKOFU.
Wahitimu wa mafunzo ya Kipaimara katika kanisa Mt Philipo Ukonga Mazizini wakimsikiliza kwa makini Askofu Mokiwa.
Wahitimu wa Kipaimara Mt St Peters Mbezi Luisi.
Watoto wa Askofu Mokiwa Joseph na Lilian wakitambulishwa na Baba Askofu kanisa la St Peter Mbezi Luisi
                                   CHAGUENI KIONGOZI  KWA MAPENZI YENU.
Askofu Mokiwa aliwasihi waumini kuchagua kiongozi kwa kufuata matakwa ya nafsi yao na si kwa kushinikizwa na mtu yoyote katika  uchaguzi mkuu ujao.
Padri Kupera akimbatiza mtoto katika kanisa Anglikana Mt Paulo Ukonga Dar es salaam
Kwaya ya Amani Mt Paulo Ukonga.

Sunday, 20 September 2015

GOODY NEWS

                             DAYOSISI YA DAR-ES-SALAAM
   KANISA ANGLIKANA                                          TANZANIA

           HABARI NJEMA

Uongozi wa kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar-es-salaam unapenda kuwataarifa waumini na watanzania kwa ujumla kuwa sasa kanisa limeanzisha Idara maalumu ya Mawasiliano itakayoshugulika na ukusanyaji wa taarifa na matukio mbalimbali ya kikanisa kisha kuyarusha kupitia mitandao ya kijamii na katika ubao wa matangazo wa Dayosisi.

Idara inaomba Maaskofu,Mapadre na Mashemasi kuwasilina na Idara hii pindi kunapokuwa na matukio muhimu ya kikanisa.
Pia tunakaribisha matangazo kwa bei nafuu.

Kwa maelezo zaidi fika ofisi kuu ya Dayosisi Ilala Dar-es-salaam au piga simu namba 0713-233575,Pia unaweza kutembelea diocesetz.blogspot.com

ASKOFU MOKIWA AONGOZA HARAMBEE.


Askofu Dakta Valentino Mokiwa akifungua kwa sala zoezi la harambee kuchangia ununuzi wa viwanja Kigango cha Makoka Ubungo Dsm tendo lililofanyika katika  mtaa wa mt Batholomayo Ubungo.
Askofu Mokiwa akiwa na Mapandre na Mashemasi waliohudhuria harambee hiyo.


Mwenyeji wa Harambee Shemasi Stephen Siwa wa kanisa Anglikana Ubungo

Meza ya uhasibu,Katika harambee hiyo Ahadi ilikuwa sh,9,765800,Zilizolipwa sh,2,686,800 na kiasi kilichobaki ni 7,079000

Kwaya ya Kanaani ikiimba katika Harambee hiyo

Peter Mamkwe,mpiga drums wa Kaanani kwaya.

Jengo la kanisa la Mt Batholomayo Ubungo Anglikana likiwa katika hatua za ujenzi


Friday, 18 September 2015

MATUKIO YA KONGAMANO LA AMANI KATIKA PICHA.

Askofu wa kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar-es-salaam Dakta Valentino Mokiwa akichangia hoja katika Kongamano la Uhuru,haki na Amani kuelekea uchaguzi mkuu lililofanyika katika ukumbi wa Blue Peal Jijini Da-es-salaam.

Inspector General wa Polisi IGP Ernest Mangu akifafanua baadhi ya hoja kaika kongamano hilo

Askofu  Dakta Valentino Mokiwa akisikiliza kwa makini hoja zilizokuwa zikitolewa katika kongamano hilo.

Profesa Baregu alikuwa ni mmoja kati ya washiriki wa kongamano hilo.

Askofu Josephat Mwingira akisistiza jambo katika kongamano hilo.

Washiriki wakiwa katika sala.

Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima Joseph Gwajima akitoa mchango wake wa mawazo katika kongamano hilo