Thursday 29 December 2016

MATUKIO MISA YA X MAS NA UTOAJI MISAADA KITUO CHA WATOTO YATIMA.

Askofu  Dr Valentino Mokiwa akimvisha kiatu mmoja wa watoto yatima wa kituo cha Valentine kilichopo Buza Dsm ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na akina Mama wa Kikristo wa kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam.[UMAKI.]

Askofu Mokiwa Akiendesha misa ya Xmas Kanisa la Mt.Cesilia Kinyerezi iliyokwenda sambamba na kupandisha Kigango hicho na kuwa mtaa kamili.

Umoja wa akina mama wa Kikristo Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam wakitoa msaada kituo cha watoto yatima kinachomilikiwa na kanisa Anglikana.


Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam latekeleza sera ya upandaji miti jiji la Dar es salaam.

Askofu Dr Valentino Mokiwa akiwa na Askofu mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania Jacob Chimeledya [kushoto]na mwakilishi toka ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam na baadhi ya watumishi wa Dayosisi wakiwa katika mazungumzo katika zoezi la upandaji miti lililofanyika viwanja vya kanisa kuu Mt.Albano Upanga Dec 2016.







Askofu Mokiwa akishirikiana na mwakilishi ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam katika zoezi la upandaji miti.

                                                               NAFASI ZA KAZI.
Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam inakaribisha maombi ya nafasi za kazi zifuatazo.
1,Mkuu wa shule ya Sekondari Buza
2,Mkurugenzi wa fedha wa Dayosisi.
3,Afisa Bima,Anglo Insuarance


Kwa maelezo zaidi fika ofisi ya Dayosisi makao makuu Ilala Amana mtaa wa Moshi au piga simu no 0713,233573.Mwisho wa kupokea maombi ni Februari 2017.

Monday 19 September 2016

ASKOFU FRITH WA DAYOSISI YA HEREFORD NCHINI UINGEREZA AFANYA ZIARA DAYOSISI YA DSM.

Askofu DR Valentino Mokiwa akiongoza ugeni wa Askofu Frith katika ofisi za Dayosisi.

Askofu Frith akisaini kitabu cha wageni ofisi ya Askofu Dayosisi ya Dar es salaam.

Askofu Frith akiongoza Misa Mtaa wa Nikolao Ilala.



Ugeni wa Askofu Frith pia ulipokelewa na wanafunzi wa shule Mtakatifu Augustino inayomilikiwa na kanisa Anglikana Dayosisi ya Dsm iliyopo Buguruni Malapa

MAENDELEO BANK WATOA MSAADA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA KANISA ANGLIKANA KIITWACHO VALENTINE CHILDRE,S HOME KILICHOPO BUZA DSM

Katibu mkuu wa Dayosisi Canon Jonathani Shenyagwa akimkaribisha Mkurugenzi wa Maendeleo Benk katika kituo cha watoto yatima cha Valentine-Buza


Mkuu wa kituo cha watoto yatima Bwana Simoni Musoke akipokea msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo unga,maharage mashuka nk toka Maendeleo Bank.

Tuesday 23 August 2016

JAJI AUGUSTINO RAMADHANI AZINDUA UJENZI JENGO LA MAKAZI YA PADRE WA MTAA,MTAKATIFU CLARA MAKONGO JUU KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA KUMI YA KANISA HILO.

Padre wa Mtaa Kelvin Ngaeje  akitoa maelekezo eneo la ujenzi.

Jaji Augustino Ramadhani akiweka jiwe la msingi ujenzi wa nyumba ya Padre wa Mtaa.

Jengo makazi ya Padre wa Mtaa,Mtakatifu Clara Makongo Juu katika hatua za ujenzi.

Sunday 24 July 2016

Marafiki wakipaka rangi jengo la kituo cha watoto yatima.

Gari lilitolewa na Dayosisi kusaidia kituo cha Yatima likiwa katika hali nzuri baada ya kukarabatiwa.

Kituo hicho pia kinaendesha miradi mbalimbali ikiwemo bustani za mboga na ufugaji.

Ma Sister ambao ndio walezi wa kituo cha yatima wakishiriki michezo na watoto hao pamoja na marafiki.





ZIARA YA MARAFIKI TOKA NCHINI MAREKANI KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA VALENTINE CHILDRENS HOME KILICHOPO BUZA DSM.WAIOMBA JAMII KUWA NA MOYO WA UPENDO KWA WATOTO HAO NA KUWASAIDIA.

Mmoja wa marafiki akiwa amembeba mtoto yatima.


Marafiki toka nchini Marekani wakiwa na watoto yatima baada ya kwenda nao eneo la michezo la FUN CITY Kigamboni ambapo walicheza nao,wakala na kunywa.



Afisa Habari wa Dayosisi Yohana Sanga kushoto akiwa na mmoja wa marafiki.

Monday 18 July 2016

WANANCHI WALISHUKURU KANISA ANGLIKANA DAYOSISI YA DAR ES SALAAM KWA HUDUMA YA MAJI.

Canon Howard Castlebery toka nchini Marekani akizindua kisima kilichopo Tuangoma ambacho amekifadhili kupitia Dayosisi ya Dar es salaam.

Katibu mkuu wa Dayosis Canon Jonathan Shenyagwa katikati  akizungumza na mkuu wa shule ya Sekondari Minaki  kulia Mwl Harold Chungu katika ziara ya uzinduzi wa kisima.


Canon Joseph Opiyo akizindua kisima kwa maombi shule ya Sekondari Minaki Kisarawe Dsm.


Canon Howard akizindua kisima.


Kisima kimezinduliwa


Bwawa la maji yaliyokuwa yanatumiwa na wanafunzi wa Minaki na wakazi wa Kisarawe ambayo si salama kwa matumizi ya binadamu.

Katibu mkuu wa Dayosisi akisalimiana na waamini wa Kianglikana kanisa la Damu ya Yesu takatifu lililopo Ruvu Stesheni kabla ya uzinduzi wa kisima.

Kisima kikifanyiwa maombi


Kigango cha Damu ya Yesu takatifu ambacho waamini wake walio wengi wana asili ya kimasai.Katibu mkuu pamoja na wafanya kazi wa Dayosisi waliokuwa katika ziara hiyo wamejitolea mifuko ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa Kigango cha kisasa.


Huduma ya uchimbaji kisima ikiendelea katika kijiji cha Kisezi wilaya Bagamoyo
Wananchi wa kijiji cha Kisezi wakilishukuru kanisa.