Friday 25 December 2015

MATUKIO YA IBADA YA KRISMASS KANISA KUU ANGLIKANA ST ALBANO UPANGA.

UJUMBE WA KRISMASS-HESHIMUNI NDOA ZENU.

Askofu wa kanisa Anglikana Dr Valentino Mokiwa  Dayosisi ya Dar-es-salaam akiongoza Ibada ya Kkrismass katika kanisa kuu la St Albano Upanga

Askofu mokiwa aliwaasa wanandoa kuheshimu ndoa zao.

Baadhi ya waumini wakishiriki Ibada.

Mpiga kinanda wa kanisa la St Albano Bwn Jeffy.
Mwinjilist Baliko akisoma neno.

MATUKIO SIKU YA MAVUNO VIWANJA VYA ST AUGUSTINE BUGURUNI.

Askofu Mokiwa akiwa na kamati ya maandalizi ya mavuno.

Askofu Mokiwa akitoa vyeti vya heshima kwa vigango na mitaa iliyovuka lengo katika uchangiaji wa mavuno

Katibu mkuu wa Dayosisi Jonathan Senyangwa akinyanyua juu kikombe cha ushindi cha uchangiaji mavuno

Wednesday 2 December 2015

VALLENTINE CHIDRENS HOME (VIDEO)



Kutokana na kuongezeka kwa watoto wa mitaani na ya yatima,Askofu wa kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar-es-salaam Dr Vallentino Mokiwa  kwa ushirikiano na wahisani kutoka nchi za nje kwa huruma yake ameamua kuanzisha kituo cha watoto yatima kiitwacho Vallentine Chidren's Home kilichopo Buza jijini Dar-es-salaam.Kituo kina watoto 19 na kinalelewa na Masister wawili.

Ili kupunguza tatizo la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, Askofu Mokiwa ameomba wadau mbalimbali yakiwemo makanisa kujitokeza kusaidia ili kupunguza tatizo hilo.

ANGALIA VIDEO HAPO CHINI


Monday 30 November 2015

MATUKIO KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA VALENTINE CHIDREN'S HOME BUZA DSM.

Jengo wanaloishi watoto yatima Valentine Chidren's home kituo  kinachofadhiliwa na Askofu Dr Valentino Mokiwa wa kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar-es-salaam na wahisani kutoka nchi za nje.

Askofu Dr Valentino Mokiwa akifurahi pamoja na watoto yatima Buza.

                                                               TUIMBE
Askofu Mokiwa akiimba na watoto yatima.

Askofu Mokiwa akitoa zawadi kwa watoto yatima.

Sister  Lucy Lipenga akihudumia kuku ikiwa ni sehemu ya mradi uliopo kituo cha Watoto yatima Buza.

Mbuzi,sehemu ya mradi uliopo katika eneo la kituo cha watoto yatima cha Valentine chidren'home.


Askofu Mokiwa akiwa na walezi wa kituo hicho.

NANI ANAJUA KUCHEZA MPIRA ?


                                                                   HAMNIWEZI!
Askofu mokiwa akicheza mpira na watoto yatima wa kituo cha Valentine Chidren's home.




kisima cha maji kinachotumia umeme wa solar kwa ajili ya kuhudumia  kituo cha Watoto yatima Valentine.




Monday 23 November 2015

MATUKIO KUWEKWA WAKFU ASKOFU JULIUS LUGENDO MKOANI MBEYA.

HONGERA ASKOFU LUGENDO


Askofu Julius Lugendo akila kiapo.

Askofu Lugendo akiendesha ibada ya chakula cha Bwana.

Askofu mstaafu kanisa Anglikana TZ akihubiri katika ibaba ya kuwekwa wakfu Askofu Lugendo.

Waumini wakiwa katika maandamano ya Ibada hiyo.

Profesa Kabudi msajili kanisa Anglikana TZ akisoma ratiba ya Ibada ya kuwekwa wakfu Askofu Lugendo.

Jopo la Mapadre waalikwa katika ibada ya kuwekwa wakfu Askofu Lugendo.

Kanisa lililofanyika Ibada ya kuwekwa wakfu Askofu Lugendo mkoani Mbeya.

Wednesday 18 November 2015

PICHA ZA MATUKIO MASHINDANO YA UIMBAJI.

Washindi wa kwanza kwaya ya  St Thomas Yombo.
WOTE MMEIMBA VIZURI
Father Jonson Lameck mratibu wa vijana wa Dayosisi akitoa neno la pongezi


                                                           TUMESHINDA.
Waalimu wa kwaya zilizoshinda wakiwa wameshika vikombe vya ushindi baada ya kukabidhiwa na Canon John Mlekano katika kanisa la Mt Albano Upanga.


 
MSHINDI NI ?
Jaji wa mashindano hayo Lazaro Mashili akitaja washindi.


Jopo la waalimu wa vikundi vya kwaya kumi na moja.



Monday 16 November 2015

MATUKIO YA KIPAIMARA MWENGE

Askofu Daktar Valentino Mokiwa kulia akiongoza waumini wa kanisa la mtaa wa Mt Petro na Paulo Mwenge kuingia katika kanisa hilo kwa ibada ya Kipaimara.

                      
                                                    BIBI APATA KIPAIMARA.


Mmoja wa wahitimu wa kipaimara Bi Ester Mongu mwenye umri wa miaka 80 akiwa katika hali ya furaha.

Bi Mongu akisaidiwa kusimama na Askofu baada ya kuwekewa mikono

Wahitimu.

Baadhi ya wafanyabiashara wa mashada wakiwa nje ya kanisa hilo.

Mwonekano wa kanisa la Mt Petro na Paulo  kwa nje likiwa katika hatua za ujenzi.

                                                        UMAKI YAPATA JENGO
Mwonekano wa jengo jipya la ofisi ya umoja wa akina Mama wa Kikristo lililojengwa kwa ushirikiano wa Dayosisi na umoja huo likiwa maeneo ya ofisi kuu ya Dayosisi.

Thursday 22 October 2015

MATANGAZO

MAANDALIZI YA KALENDA.


Ofisi ya Dayosisi inaomba Mitaa kuleta picha Idara ya Habari hapa Dayosisi kwa ajili ya kuandaa Kalenda ya mwaka 2016 kabla ya tarehe 30 Nov 2015.

ALMANAC.


Ofisi ya Dayosisi imeanza kuandaa ALMANAC ya mwaka 2016.Mitaa inaombwa kuwasilisha ratiba za matukio kabla ya tarehe 30 Nov 2015,hapa Idara ya Habari na Mawasiliano Dayosisi .

BIMA


Pia Dayosisi inawatangazia waumini na Watanzania wote kuwa Idara yake ya Bima (ANGLO INSURANCE AGENCY) imeendelea kutoa huduma zake za bima za kawaida na maisha(General and life assurance)ikiwemo bima za magari,nyumba,afya,biashara,elimu,maisha,ajali,majaliwa,n.k.

                          KARIBU UPATE HUDUMA BORA.

KITUO CHA AFYA BUGURUNI ANGLIKANA CHAZIDI KUBORESHA HUDUMA ZAKE ZA AFYA.




Mtoto akipimwa uzito



Mkurugenzi wa kituo cha Afya Buguruni Anglikana DR Simon Walton.
Mmoja wa Madaktari wa kituo hicho akifanya vipimo katika maabara.

Moja ya chumba kilicho katika matayarisho ya utoaji wa huduma za upasuaji.